Unajimu au astrolojia ni
elimu juu ya uhusiano kati ya nyota na maisha ya binadamu duniani.
Wanazuoni wa unajimu wanaeleza ya kwamba nyota zinaathiri maisha ya watu
na matukio kama amani, vita au maafa. Mahusiano haya hayajaweza
kuthibitishwa na sayansi ya fizikia au sayansi nyingine. Alama za nyota
12 ni msingi wa falsafa hii ya unajimu.
Astrologia imekuwa ikitumika kwa miaka mingi lakini siku zote imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka kwa wana sayansi.
Astrolojia ina misingi tokea enzi za zamani wakati sayansi ilipokuwa
ya chini na imani za kiroho na kiungu zikiwa za kiwango cha juu katika
jamii nyingi.
Baadhi ya tafiti zilizofanywa kuchunguza usahihi wa astrolojia
unaonyesha kuna usahihi wa asilimia kama 3o tu. Hii si haba,kuna ukweli
basi katika hili japo bado kuna upinzani mkubwa toka katika ulimwengu wa
sayansi ya kisasa
Tabia za Watu na Alama za Nyota
Alama za nyota zinabashiri tabia na haiba ya binadamu katika dunia.
Mpangilio au nafasi ya sayari katika mzunguko wake angani unaaminika
kuleta athari kwa binadamu na matukio katika dunia.
Kuna alama 12 za kiastrolojia. Kila moja ina mvuto wa nguvu wa kipekee toka katika nyota.
Alama hizi ni kama ifuatavyo:
- Waliozaliwa Feb 19 – Machi 20 wana nyota ya Samaki (Pisces)
- Waliozaliwa Machi 21 – Aprili 19 wana nyota ya Kondoo (Aries)
- Waliozaliwa Aprili 20 – Mei 21 wana nyota ya Ng’ombe (Taurus)
- Waliozaliwa Mei 22 – Juni 20 wana nyota ya Mapacha:(Gemini )
- Waliozaliwa Juni 21 – Julai 22 wana nyota ya Kaa(Cancer)
- Waliozaliwa Julai 23 – Agosti 22 wana nyota ya Simba(Leo)
- Waliozaliwa Agosti 23 – Sept 22 wana nyota ya Mashuke(Virgo)
- Waliozaliwa Sept 23 – Okt 22 wana nyota ya Mizani (Libra)
- Waliozaliwa Okt 24- Nov 21 wana nyota ya Ng’e (Scorpio)
- Waliozaliwa Nov 22- Des 21 wana nyota ya Mshale (Sagittarius)
- Waliozaliwa Des 22 – Jan 19 wana nyota ya Mbuzi(Capricorn)
- Waliozaliwa Jan 20 – Feb 18 wana nyota ya Ndoo (Aquarius)
Makundi ya Alama za Nyota:
Alama hizi 12 za nyota zinagawanyika katika sehemu kuu 4 zijulikanazo kama:
- Moto:Yenye matamanio ya mafanikio au makuu,dadisi
- Maji:Yenye kubadilika na yenye uwezo wa ufahamu wa ndani
- Hewa:Imara na yenye kukuza au kuendeleza
- Udongo:Yenye elimu au uwezo wa kutambua na yenye kuhamasisha
Hizi ni sehemu nne zinazoongoza astrologia. Kila kimojawapo kinabeba tabia fulani.
Alama hizi 12 za nyota zimegawanyika kama ifuatavyo:
- Moto: Kondoo, Simba,Mshale
- Maji: Ng’e, Samaki, Kaa
- Hewa: Mapacha, Mizani, Ndoo
- Udongo: Ng’ombe,Mashuke,Mbuzi
Kila alama ya nyota 12 zimegawanyika pia katika makundi mengine matatu ambayo ni:
- Yenye Umuhimu au Msingi “Cardinal”: Kondoo, Kaa,Mizani,Mbuzi
- Yenye Kubadilika “Mutable”: Ng’ombe, Simba, Ng’e na Ndoo
- Isiyobadilika “Fixed”: Mapacha, Mizani, Mshale na Samaki
Alama ambayo iko katika moto na iko katika kundi la msingi huwa na tabia za upinzani na ubishani wa hali ya juu kama Kondoo
Alama ambayo ipo katika kundi la Udongo na Kubadilika huwa na tabia za utulivu wa hali ya juu kama Ng’ombe.
Haiba na Tabia za Alama za Nyota
1 Nyota ya Kondoo
- Ni mwenye maamuzi yasiyopinda na mtendaji mzuri wa kazi.
- Anategemea makuu juu yake mwenyewe na kutoka kwa wengine
- Mwenye kujitegemea na mwenye ari ya hali ya juu
- Anauthubutu wa kujaribu mambo makubwa
- Mwenzilishi wa mambo na mbunifu
- Kiongozi
- Muongeaji
- Ni mwenye hisia kali na asiye na uvumilivu mkubwa.
- Mwaminifu kwa marafiki na familia
- Anajali mpenzi wake na mwenye hisia kali za mapenzi
2 Nyota ya Ng’ombe
“Nafanya ninachokipenda” Nimepata.
- Ni mwenye nguvu na mstahimilivu kimwili na kiakili
- Makini na muangalifu
- Ana kiburi na asiyekubali kushindwa kirahisi
- Mstahimilivu
- Mwenye kutegemewa
- Ni mgumu kubadilika
- Anapenda vitu vizuri na vya thamani
- Unapenda urembo na vitu vya kupendeza
- Mwenye hisia zilizofichika
- Huenda akaonekana mbinafsi lakini ni wenye kutoa wakiwa na mali au fedha.
3 Nyota ya Mapacha
Ninafikiri, Nadhani “Ninapanga” Ndugu zangu
- Ni mwenye kipaji kikubwa,mwenye kubadilika na anayechoka haraka na kukata tamaa
- Anafikiri kwa haraka na mcheshi
- Ni mwasilianaji mzuri
- Ni mtu anayependa watu na mwenye kupenda mabadiliko.
- Mwenye kuamua kwa akili na mbunifu
- Hana utulivu
- Ana mipango na malengo makubwa
- Mwenye kubadilika kirahisi
4 Nyota ya Kaa
Ninahisi, Nasita, Nakwama
“Nina wasiwasi kuhusu Jambo”Naogopa
- Anapenda kukaa nyumbani na kuwa na makazi mazuri yenye kumpautulivu ,usalama na amani
- Anapenda marafiki na familia. ANanpenda kufuatilia historia ya ukoo
- Hisia zake ni za wazi na ni rahisi kujulikana
- Ana huruma
- Ni mwangalifu
- Mkimya na
5 Nyota ya Simba
Nitafanya, Nitaanza
“Najifanya” Nitasingizia
- Kama alivyo simba ni jasiri na mwenye uthubutu.
- Anapenda kuonekana na watu
- Sanaa ni mojawapo ya maeneo ambayo anayamudu na ambayo yanamfanya afanikiwe
- Wana maamuzi mazuri na ni waigizaji mahiri.
- Ni wenye moyo wa kutoa na wenye upendo mkubwa
- Ni viongozi wazuri na wenye nguvu
- Mwenye matumaini mazuri
- Mwenye kuheshimika
- Mshindani
- Mpangiliaji mzuri wa mambo ya kufanya
- Mwenye mvuto
6 Nyota ya Mashuke
Ninasoma, Nasikitika, nakula, naumwa,Naonewa
“Nina khofu” nitakunywa, nasingiziwa, napoteza, nakunywa dawa, kelele nyingi.
- Ana mategemeo makubwa juu yake mwenyewe na kutoka kwa watu wengine
- Ni mwenye ujuzi na mwenye mafanikio makubwa kazini
- Ni mchunguzi na mdadisi wa mambo na mwenye kufanya kitu kimoja kwa wakati mmoja.
- Wapangili wazuri wa muda na watekelezaji
- Ni mdadisi na mbishi katika kuhakikisha mambo yanafanyika kwa ukamilifu.
- Ni wafanya kazi wenye umakini na ni waangalifu katika kazi zao.
- Wanajali afya
7 Nyota ya Mizani
Ninashirikiana, Nakusanya, Naimba,Napenda, Nakumbatia“Nafanya mambo nisiyoyapenda” Nachumbia naunganisha.
Ni alama ya hewa. Mwenye nyota ya mizani anatumia muda mwingi katika kuleta usawa na haki na kusuruhisha migogoro.
Mizani anatumia akili zaidi kuliko nguvu za mwili.
- Husimamia haki na usawa
- Anapenda sanaa na urembo
- Wabunifu wa sanaa
- Ni mpenzi wa muziki
- Ni muwazi katika kuonyesha upendo
- Ana ustadi wa kukabiliana na mambo ya kijamii
- Anatoa matazamo wake pale tu anapochokozwa au anapoguswa kihisia
- Mpenda amani
- Wenye mvuto wa kupendwa
8 Nyota ya Ng’e
Nataka kufanya, Natamani, Nadhibiti. “Ninashuku”Ninahusudu.- Anapenda mambo makubwa na maisha ya mazuri
- Mjasiriamali namwenye uwezo wa kukabiliana na vizingiti vikubwa
- Anapenda malumbano makali
- Wanatumia nguvu
- Jasiri
- Wastahimilivu
- Washindani
- Wanauwezo ,
- Wachunguzi wa mambo
- Wasiri
- Ni mpenzi mzuri na mwenye tabia za umiliki
- Wanajitegemea
- Ni wenye maamuzi
9 Nyota ya Mshale
Ninaelewa, Nafahamu yote, hakuna Nisilojua
- Mwanafalsafa na mkusanyaji wa habari
- Mwenye uwezo mkubwa kiakili ma anapenda changamoto
- Ni mwenye nguvu ambazo humfanya mara zote aende mbele.
- Ni mwenye kupenda uhuru
- Ni mpenzi mwenye mvuto na anapenda kumridhisha mpenzi wake
- Rafiki
- Mwenye ari
- Hawana utulivu
- Waaminifu na wakweli
- Wanapenda safari
10 Nyota ya Mbuzi
Ninatumia, Nimezoea, naongoza “Sijiamini” Nimebanwa
- Mwenye malengo , mipango na matarajio makubwa
- Ni mtatuaji wa matatizo kwa vitendo na mapangiliaji mzuri wa mambo-Mtendaji
- Ni mwenye mipango na mfuatiliaji wa mipango yake
- Si mshirikishaji mzuri mpaka aombwe au asukumwe.
- Ni mpenzi mzuri na rafiki wa maisha
- Mgumu kubadilika
- Mbishi na asiyekubari kushindwa kirahisi
- Mfanyabiashara
- Mwajibikaji
11 Nyota ya Ndoo
Ninajua, Nathibitisha “Usinitegemee”Nitakwepa- Ni mbinafsi na asiyependa kufuata utaratibu au sheria.
- Wakipekee
- Anaejitegemea na hupenda kuwa peke yake
- Mwenye huruma
- Muona mbali
- Mwenye ufahamu wa hali ya juu nma mbunifu
- Anafanya marafiki wa aina mbalimbali
- Ana utu na mwenye kudai haki
- Anapendwa na watu na anategeneza urafiki kwa haraka
- Anapenda sanaa na maisha ya anasa.
12 Nyota ya Samaki
Ninaamini, Ninaota “Ninakwepa”- Ni mkweli na mwenye hisia nzito
- Hana ubinafsi
- Ni mpenzi mwaminifu na rafiki
- Mpenda amani
- Ana huruma
- Anajitoa
- Wana ndoto
- Wabunifu
- Wana aibu
16 comments
Am leo but I like so much fun and travel what's up with this?
Mm siijui nyota yangu.
Nimependa sana maelezo
Nimependa sana maelezo
Mtu mwenye nyota ya mbuzi anaweza kumuoa mtu mwenye nyota ya ng'ombe na ndoa ikadumu?
I like thi page
kuna maelezo mazuri lakini hamjachambua kiundani zaid
Vyote Ni vya kweli katika haya asant sana
Mashuke
Mashuke
Mm ninanyota ya samaki kweli vyote hivyo ninavyo
How about you
Yes
Vina ukweli ndani yake
Iko pouwa kabisa
Kwenye nge hapo nadhani ndio umeenda chaka.
EmoticonEmoticon